• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yataka kuimarisha uhusiano wa kunufaishana kati yake na China

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:47:12

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Bw. Augustine Mahiga amesema, akiwa waziri wa mambo ya nje wa kwanza kutoka nchi za Afrika Mashariki kufanya ziara nchini China baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC kufanyika, anataka kuimarisha uratibu na ushirikiano na China kupitia ziara hiyo, ili kuimarisha uhusiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili na kusukuma mbele kwa pamoja kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatima ya pamoja.

    Waziri Mahiga amefanya ziara rasmi ya siku nne nchini China kuanzia jumatatu wiki hii. Bw. Mahiga amesema, hivi sasa rais John Magufuli wa Tanzania anaongoza wananchi kuimarisha ujenzi wa miundombinu, kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nje, na kuhimiza mchakato wa maendeleo ya viwanda. Mitindo na uzoefu wenye mafanikio wa China katika mageuzi na ufunguaji mlango na ujenzi wa kiuchumi nchini China unaweza kuisaidia Tanzania kuepuka mizunguko na kuinua uwezo wa kujiendeleza. Anasema,

    Bw. Mahiga amesema, China siku zote ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara, mkandarasi mkubwa na chanzo kikuu cha uwekezaji kwa Tanzania. Amezitaka pande hizo mbili kuzidi kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kuisaidia Tanzania kupata maendeleo mapya. Anasema,

    Pia amesema, China inashikilia wazo la usawa kati ya nchi tajiri au maskini, kubwa au ndogo, na kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na nchi mbalimbali kupitia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Ameongeza kuwa anatarajia mkutano wa 7 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwakani nchini China utazidi kuhimiza uhusiano wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako