• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kazi ya uchumi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:50:13

    Mkutano wa siku tatu wa kazi ya uchumi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umefanyika kuanzia tarehe 18 mwezi huu hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati hiyo amefanya majumuisho kuhusu mchakato wa maendeleo ya uchumi wa China baada ya mkutano mkuu wa 18 wa CPC kufanyika, kuchambua hali ya uchumi ya hivi sasa, na kuweka mpango kuhusu kazi ya uchumi ya mwaka ujao.

    Mkutano huo umesema, uchumi wa China umeingia kwenye kipindi cha maendeleo yenye ubora kutoka kipindi cha maendeleo ya kasi. Kuhusu kazi ya uchumi ya mwaka 2018, mkutano huo umesisitiza kuwa kauli mbiu ya jumla ya kazi hiyo, ambayo ni kupata maendeleo juu ya msingi wa kukuza uchumi kwa utulivu itadumishwa kwa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako