• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Marekani asema China haina nia ya kuongoza dunia

    (GMT+08:00) 2017-12-21 16:50:36

    Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai ameeleza maoni yake juu ya mkakati wa usalama wa taifa uliotolewa hivi karibuni na serikali ya rais Donald Trump, na kusisitiza kuwa China haina nia ya kuongoza dunia.

    Balozi Cui Tiankai amesema hayo alipohojiwa na kituo cha habari cha CNN cha Marekani. Amesema ripoti moja ya kimkakati inatakiwa kuonesha kanuni tatu, ambazo ni maono halisi ya kimataifa, upeo wa kuona mbali na msimamo wa kiujenzi na kiushirikiano, hivyo ripoti iliyotolewa na Marekani bado inatakiwa kuboreshwa kwa pande hizo tatu.

    Balozi Cui amesema, nchi mbalimbali zinakabiliwa na changamoto za pamoja, pia zina maslahi ya pamoja yanayozidi kuongezeka siku hadi siku, hivyo China inaona kuwa ni muhimu kujenga uhusiano wa kiwenzi unaoshirikisha pande nyingi duniani, na kukabiliana na changamoto kwa pamoja. Lengo la China ni kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatima ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako