• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema lengo la uhusiano wa kiuchumi wa kibiashara si kushindana bali ni kupata mafanikio kwa pamoja

    (GMT+08:00) 2017-12-21 17:33:30

    Wizara ya mambo ya nje ya China imesema uhusiano wa kiuchumi wa kibiashara hauwezi kuchukuliwa kuwa mashindano, na lengo la uhusiano wa kimataifa wa aina mpya ni kufanya ushirikiano na kupata mafanikio kwa pamoja.

    Kauli ya wizara hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Marekani kutoa ripoti ya kwanza ya mikakati ya usalama ya kitaifa, na kusema Marekani italinda maslahi yake ya kiuchumi, na kuichukulia China kuwa mshindani wa kimkakati. Msemaji wa wizara hiyo Bw. Gao Feng amesema China inazichukulia Marekani na wenzi wengine wa kiuchumi na kibiashara kuwa washirika badala ya washindani, na China haijawahi na kamwe haitatekeleza sera ya uvamizi wa kiuchumi.

    Akizungumzia muswada wa marekebisho ya njia ya kuchunguza bidhaa zinazouzwa kwa bei nafuu kupita kiasi uliotolewa hivi karibuni na Umoja wa Ulaya, na ripoti inayodai kuwa soko la China limepotoshwa, Bw. Gao amesema China itaweza kutumia mamlaka zake husika za kutatua mgogoro wa kibiashara kwenye msingi wa Shirika la Biashara Duniani, na kuchukua hatua kulinda kithabiti haki na maslahi yake halali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako