• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meli yazama nchini Ufilipino na kuua watu wanne

    (GMT+08:00) 2017-12-21 19:15:44

    Meli iliyokuwa imebeba watu 251 imezama katika jimbo la Quezon nchini Ufilipino kutokana na mawimbi makali, na kuua watu wasiopungua wanne.

    Afisa Utawala wa hospital ya wilaya Infanta huko Quezon, Bw. Claro Reto, amesema wapo pia manusura 11 waliofikishwa hospitalini hapo.

    Naye msemaji wa kikosi cha uokoaji, Armand Balilo amewaambia waandishi wa habari kuwa, wao watafuatilia na baadaye kuthibitisha kuhusu taarifa za baadhi ya abiria kudaiwa kuwa wamezama.

    Msemaji huyo pia amesema meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 286 ilizama saa moja baada ya kuanza safari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako