• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa UN aitisha duru mpya ya mkutano kuhusu suala la Syria mwezi Januari

    (GMT+08:00) 2017-12-22 09:02:23

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia suala la Syria Bw. Staffan de Mistura amesema anapanga kuitisha duru ya tisa ya mazungumzo kuhusu suala la Syria mjini Geneva mwezi Januari mwakani. Bw. Mistura ametangaza mpango huo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Moscow baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Bw. Sergei Shoigu. Amesema duru mpya ya mazungumzo itafuatilia njia za kutekeleza kikamilifu Azimio No. 2254 la Baraza la usalama lililopitishwa Desamba mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako