• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya warefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia kwa miezi sita

    (GMT+08:00) 2017-12-22 10:12:52

    Baraza la Umoja wa Ulaya limeamua kurefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia kwa miezi sita zaidi, hadi tarehe 31 mwezi Julai mwakani.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo kwenye mkutano wa Umoja wa Ulaya uliofanyika tarehe 14 mwezi huu inasema, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel waliwaarifu viongozi wengine wa nchi wanachama wa Umoja huo kuhusu hali ya utekelezaji wa makubaliano ya Minsk, na kuona kuwa Russia haitekelezi makubaliano hayo.

    Tangu mwaka 2015 Umoja wa Ulaya umerefusha muda wa vikwazo vya kiuchumi mara kadhaa, kutokana na makubaliano ya Minsk kutotekelezwa kikamilifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako