• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi ya milioni 40 wakabiliwa na njaa kutokana na machafuko Mashariki ya Karibu

    (GMT+08:00) 2017-12-22 10:13:29

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwaka huu na Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO kuhusu usalama wa chakula na lishe, watu zaidi ya milioni 40 wanakabiliwa na njaa katika nchi za NENA ambazo ni pamoja na baadhi ya nchi za Mashariki ya kati na Afrika Kaskazini, kutokana na vita na migogoro.

    Ripoti inasema watu milioni 40.2 wanakabiliwa na njaa na utapiamlo, na wengine milioni 55.2 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na migogoro katika maeneo hayo.

    Mkurugenzi mkuu wa FAO Bw. Abdessalam Ould Ahmed amesema mwaka huu ripoti ya FAO inaonyesha kuwa migogoro ndiyo chanzo kikuu cha hali ya kushuka kwa usalama wa chakula na lishe katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako