• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xavi asema Messi ni hatari zaidi kuliko Cristiano kisoka

  (GMT+08:00) 2017-12-22 10:23:25

  Kauli aliyoitoa Cristiano Ronaldo baada ya kutwaa tuzo ya Ballon D Or. Kwamba yeye ni mwanasoka aliyekamilika, mwanasoka bora katika historia ya soka na amefanya mengi ambayo sio rahisi kufanyika, imepingwa sana na kiungo wa zamani wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez ambaye amesema anashukuru kwa kumuona Ronaldo akicheza soka na pia amemuona Lioneil Messi lakini amekiri Messi ni hatari zaidi kuliko Cristiano.

  Xavi anasema katika soka hakujawahi kutokea mchezaji kama Lioneil Messi, na Cristiano Ronaldo kama anaona yeye ni bora basi aamini hivyo lakini watu wanaotazama soka yao wanaona Messi ni zaidi.

  Jumamosi hii wawili hao wataoneshana umwamba huku Messi akiwa amefunga mabao 18 katika michezo 24 msimu huu na Cristiano Ronaldo akiwa amefunga mabao 16 katika michezo 21 msimu huu.

  Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na alama 42 kileleni huku wapinzani wao Real Madrid wako nafasi ya nne wakiwa na alama 31 ikiwa ni alama 11 nyuma ya Real Madrid na El Classico inaweza kushuhudia pengo la alama kuongezeka ama kupungua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako