• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wajadili jinsi ya kufanya uchumi wa China kukua kwa ubora

    (GMT+08:00) 2017-12-22 16:13:03

    Wataalamu na maofisa wa sekta ya uchumi wamekutana hapa Beijing na kujadili jinsi ya kufanya uchumi wa China kukua kwa ubora, badala ya kuzingatia kasi ya ongezeko la uchumi.

    Akizungumza katika kongamano hilo, mchumi mkuu wa idara ya takwimu ya China Sheng Laiyun amesema idara hiyo itatumia msimamo mpya kutoa viashiria mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya uchumi yenye ubora. Anasema, "Kwanza tunapaswa kuacha kuzingatia sana kasi ya ongezeko la uchumi. Tofauti na siku zilizopita ambapo tulitaka upanuzi mkubwa na wa kasi wa maendeleo ya kiviwanda, sasa mazingira ya ndani na nje ya maendeleo ya uchumi yamebadilika, na ni vigumu kufanya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa sasa kifikie kile cha zamani. Tunapaswa kupunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi, hii inatusaidia tuangalie zaidi mabadiliko ya muundo wa kiuchumi na jinsi ya kujiendeleza."

    Kongamano hilo limefanyika baada ya mkutano wa kazi za uchumi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China uliomalizika hivi karibuni kudhirisha kuwa, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa China yenye ubora ni msingi wa kutunga mipango ya maendeleo kwa sasa na siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako