• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuvipigia kura vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-12-22 16:48:59

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura kuhusu muswada mpya wa azimio litakaloweza kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwa ni kujibu jaribio la makombora lililofanywa na nchi hiyo mwezi uliopita.

    Baraza hilo linatarajiwa kukutana leo kupitia muswada wa azimio lililoandikwa na Marekani kuhusu suala hilo.

    Wakati huohuo, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema kuwa serikali yake imefanikiwa kuendeleza nguvu zake za nyuklia licha ya matatizo inayokabiliwa nayo.

    Akizungumza kwenye mkutano wa chama tawala cha Wafanyakazi nchini humo, rais Kim amesema nchi yake imetekeleza kikamilifu sera za uhuru kwenye siasa, kujitosheleza kiuchumi, na kujitegemea katika ulinzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako