• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vitendo vyovyote dhidi ya raia vinavyochochea mgogoro

    (GMT+08:00) 2017-12-22 18:42:22

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying leo amesema, China siku zote inapinga vitendo vyovyote dhidi ya raia vinavyozidisha mgogoro, na kusema ni muhimu kuhimiza pande zinazopambana nchini Yemen zifikie utatuzi unaoridhisha pande zote kwa njia ya mazungumzo.

    Bi Hua amesema hayo baada ya hivi karibuni Saudi Arabia kuzuia kwa mara nyingine kombora lililorushwa na waasi wa Houthi nchini Yemen dhidi ya Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia. Saudi Arabia imesema, waasi wa Houthi waliyalenga maeneo wanayoishi raia mjini Riyadh, kitendo kinachokiuka maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu, pia kimetishia usalama wa Saudi Arabia, wa kikanda na wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako