• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yapongeza azimio kuhusu Jerusalem lililotolewa na Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-12-22 19:08:08

    Ikulu ya Palestina imelipongeza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kupitisha azimio kuhusu suala la hadhi ya Jerusalem.

    Azimio hilo limesema, uamuzi wowote au hatua yoyote inayodai kubadilisha hadhi ya Jerusalem ni batili, lakini tofauti na azimio lililotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, azimio hilo halina nguvu ya kisheria, lakini lina ushawishi wa kisiasa na kijamii.

    Msemaji wa ikulu ya Palestina Bw. Nabil Abu Rudeineh amesema, azimio hilo limethibitisha tena kuwa jumuiya ya kimataifa inaunga mkono haki ya watu wa Palestina, na pia limethibisha kuwa shughuli za kutetea haki za Palestina zinaungwa mkono na sheria ya kimataifa.

    Habari nyingine zinasema kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Lebanon, hivi sasa wakimbizi zaidi ya laki 1.7 wa Palestina wanaishi nchini humo, idadi ambayo ni kubwa kuliko ilivyokadiriwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako