• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha China cha kutengeneza vifaa vya ujenzi kuanza kazi rasmi Machi mwakani

    (GMT+08:00) 2017-12-22 20:03:14

    Kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ujenzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na duka la kuuza vifaa hivyo kwa jumla kinatarajiwa kuanza uzalishaji ifikapo machi mwaka ujao. Tangazo hili linakuja wakati ambapo serikali imekuwa ikitoa msukumo wa kupunguza gharama ya ujenzi wa nyumba kwa asilimia 40. Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya ujenzi ya China Wuyi, waziri wa biashara na viwanda wa Kenya Bw And Mohammed kiwanda hicho mbali na kupunguza gharama ya vifaa vya ujenzi pia kitasaidia kupunguza gharama ya wafanyi kazi. Ameongeza kuwa kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakilalamikia gharama ya juu ya ujenzi lakini pindi kiwanda hicho kitakapokamilika basi kutakuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye sekta ya ujenzi. Duka hilo la jumla la vifaa vya ujenzi linajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 10 za Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako