• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wastani wa ongezeko la bajeti kwa shughuli za elimu nchini China wafikia karibu asilimia 8 kwa mwaka

    (GMT+08:00) 2017-12-23 18:40:08

    Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, wastani wa ongezeko la bajeti kwa shughuli za elimu nchini China umefikia asilimia 7.9 kwa mwaka, na kiwango cha elimu cha China kimeinuka na kuwa katika nafasi ya juu ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.

    Baraza la serikali la China leo limekabidhi ripoti kuhusu bajeti ya shughuli za elimu kwa baraza la kudumu la bunge la umma la China. Takwimu zilizotolewa katika ripoti hiyo zinaonesha kuwa, China imeongeza mfululizo bajeti kwa ajili shughuli za elimu, na kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya elimu zilikuwa karibu yuan trilioni 17, sawa na dola za kimarekani trilioni 2.6.

    Takwimu hizo zinaonesha kuwa kiwango cha elimu cha China kinashika nafasi ya juu ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, na wananchi wanaelimika vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako