• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya "Jiaolong" AG600 ya China yafanikiwa kuruka kwa majaribio

    (GMT+08:00) 2017-12-24 18:20:49

    Ndege ya "Jiaolong" AG600 ambayo ni ndege kubwa zaidi inayoweza kutua nchi kavu na majini ambayo imebuniwa na kutengenezwa nchini China leo imefanikiwa kuruka kwa majaribio.

    Ndege hiyo ni kwa ajili ya kukabiliana na ajali za moto misituni, na uokoaji watu majini. Inaweza kuvuta maji tani 20 ndani ya sekunde 20, na kuzima moto katika eneo la mita za mraba zaidi ya 4,000 mara moja, huku ikiweza kuwaokoa watu 50 baharini mara moja. Mbali na kuzima moto na kuwaokoa watu, pia inaweza kutumiwa katika uchunguzi na uhifadhi wa mazingira baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako