• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kongo Brazzaville na jeshi la upinzani zasaini makubaliano ya kusimamisha vita

    (GMT+08:00) 2017-12-24 18:30:12

    Serikali ya Kongo Brazzaville tarehe 23 ilisaini makubaliano na jeshi la upinzani la Ninjas, ambapo pande hizo mbili zitaunda tume ya ushirikiano kutokana na makubaliano hayo ili kusimamia utekelezaji wa makubaliano.

    Wajumbe wa pande hizo mbili siku hiyo walifanya mkutano na waandishi wa habari huko Brazzaville.

    Makubaliano ya kusimamisha vita yalilitaka kundi hilo lisalimishe silaha zake, na kwamba haliwezi kuzuia kuunda utaratibu mpya wa taifa, na serikali imeahidi kuwapanga katika utaratibu mpya wapiganaji wa kundi hilo kwa muafaka baada ya mchakato wa kusalimisha silaha zao.

    Makubaliano hayo pia yalitaka kuwekwe utaratibu juu ya wakimbizi waliotokana na mgogoro kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako