• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Zimbabwe ateuliwa kuwa makamu wa rais wa chama tawala

    (GMT+08:00) 2017-12-24 18:30:48

    Mkuu wa zamani wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga ameteuliwa kuwa makamu wa rais na katibu wa pili wa chama tawala cha ZANU-PF.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa rais wa Zimbabwe George Charamba, Chiwenga ambaye alistaafu kuwa mkuu wa majeshi juma lililopita baada ya kukamilisha shughuli iliyosababisha rais Mugabe kujiuzulu, na ameteuliwa katika nafasi hizo mpya pamoja na aliyekuwa waziri wa ulinzi na mwanajeshi wa zamani Kembo Mohadi.

    Mohadi ni mwanachama wa zamani wa chama cha PF-Zapu kilichokuwa kikiongozwa na makamu wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Joshua Nkomo ambaye baadaye alikubaliana na hoja ya kukiunganisha chama hicho na Zanu-PF ya Mugabe ili kuunda Zanu-PF ya muungano.

    Uteuzi wa wawili hao sasa unakamilisha nafasi za makamu wawili wa Rais wa Zimbabwe zilizokuwa wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako