• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watano wauawa kwenye shambulizi la IS kaskazini mwa Iraq

    (GMT+08:00) 2017-12-25 08:48:28

    Watu watano akiwemo ofisa wa polisi, wameuawa kwenye shambulizi la ghafla lililofanywa na wapiganaji wa Kundi la Islamic State jimboni Kirkuk, kaskazini mwa Iraq. Chanzo cha habari kinasema wapiganaji wa IS waliweka kituo feki cha ukaguzi kwenye barabara inayounganisha miji ya Ryadh na Hawijah iliyoko kusini magharibi mwa jimbo la Kirkuk, na kuzuia gari moja lililokuwa na watu watano, akiwemo kanali Fedhel al-Sab'awi, mkuu wa kituo cha polisi, na kuwaua wote kwa kuwapigia risasi. Vikosi vya usalama vimeanzisha msako dhidi ya washambuliaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako