• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kufungua kituo cha viwanda vya dawa kilichojengwa na China

    (GMT+08:00) 2017-12-25 08:57:56

    Serikali ya Ethiopia itafungua kituo cha viwanda vya dawa cha Kilinto kilichojengwa na China, kinachotarajiwa kuwa na viwanda mbalimbali vya dawa. Meneja wa ujenzi wa mradi wa kituo hicho Bw Getahun Agnew, amesema asilimia 75 ya mradi tayari imekamilika.

    Ethiopia inaendelea na ujenzi wa vituo 15 vya maeneo ya viwanda, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuifanya nchi hiyo iwe kituo cha viwanda vyepesi barani Afrika kabla ya mwaka 2020.

    Habari pia zinasema serikali ya Ethiopia imetangaza mpango wa kujenga vituo maalum vya afya kwa ajili ya matibabu ya saratani. Wizara ya afya ya nchi hiyo imetenga dola milioni 80 za kimarekani kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Vituo hivyo vinatarajiwa kukamilika mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako