• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti mpya wa ANC aahidi kubadilisha uchumi wa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-12-25 09:08:54

    Mwenyekiti mpya wa chama cha ANC Bw Cyril Ramaphosa ameahidi kuubadilisha uchumi wa Afrika Kusini.

    Katika ujumbe wake wa Krismas kwa taifa Bwana Ramaphosa amesema wanapaswa kushirikiana na wenzi wa kijamii kuondoa vizuizi vyote ili kuwekeza na kuifikisha Afrika kusini katika kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi. Amesema licha ya maendeleo yaliyopatikana katika maeneo mengi muhimu kwa mwaka huu, bado wanashuhudia athari kubwa za ukosefu wa ajira kwa watu, familia na jamii. Takwimu zinaonesha kuwa kutokana na ukuaji mdogo wa uchumi, kiwango cha ukosefu wa ajira kipo kwenye asilimia 27.7.

    Katika kipindi cha mwaka mpya Bw. Ramaphosa amewataka wananchi wafanye juhudi ili kujenga jamii ambayo watu wanajiona salama na kuthamaniwa na kuendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa nguvu na kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako