• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Uturuki zasaini makubaliano 12 katika ushirikiano wa kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni

    (GMT+08:00) 2017-12-25 09:37:34

    Sudan na Uturuki zimesaini makubaliano 12 ili kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni.

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye yuko ziarani nchini Sudan kujadili njia za kuendeleza uhusiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali.

    Pande hizo mbili pia zimekubaliana kuanzisha baraza la pamoja la ushirikiano wa kimkakati linaloongozwa na viongozi wa nchi hizo mbili. Rais al-Bashir amesema ziara ya rais Erdogan imeinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako