• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yaionya Israel kwa mpango wake wa ujenzi wa makazi mapya

    (GMT+08:00) 2017-12-25 09:45:50

    Palestina imelaani vikali Israel kwa mpango wake wa kujenga makazi mapya elfu 300 mashariki mwa Jerusalem.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje na uhamiaji ya Palestina, imesema mpango huo wa Israel umekuwa sehemu ya mipango yake ya ukoloni na upanuzi, ambayo inaungwa mkono na rais Donald Trump wa Marekani kutokana na kutangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Shirika la ukombozi la Palestina PLO limeonya athari zinazoweza kutokana na mpango wa Israel kuhusu mji wa Jerusalem, ambao unalenga kuyaunganisha makazi mengi zaidi na kukalia Ukingo wa Magharibi. Na chama cha Fatah cha Palestina kimesema baraza lake litatafakari upya mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.

    Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba Israel itajitoa kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ndani ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako