• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wasema uwiano wa biashara utakuwa umbo la mwanzo la sera ya biashara ya China

  (GMT+08:00) 2017-12-25 16:07:06

  Mkutano wa mwaka wa kazi za uchumi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliomalizika hivi karibuni hapa Beijing, umetoa agizo la kuhimiza kuundwa kwa muundo mpya wenye uwazi kamili. Wachambuzi wa mambo ya uchumi wa China wanaona kukamilisha mazingira ya kibiashara ni hatua muhimu wa China kuvutia uwekezaji kutoka nje, na kuwa nchi inayowekezwa zaidi na pia kukamilisha muundo mpya wenye uwazi kamili.

  Mkutano huo wa CPC umesisitiza kuhimiza biashara yenye uwiano, kuongeza ubora na nyongeza ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya China, kupanua uagizaji bidhaa kutoka nje na kupunguza ushuru kwa baadhi ya bidhaa. Mtaalamu wa taasisi ya biashara ya kimataifa na ushirikiano wa kiuchumi katika Wizara ya Biashara ya China Bw. Huo Jianguo anaona kuwa maagizo hayo ni "umbo la mwanzo" la sera ya biashara ya China. Anasema,"Serikali ya China haijawahi kudhihirisha wazi sera yake ya biashara. Naona maagizo hayo yanaweza kuchukuliwa kama ni hatua ya kwanza, na yameweka msingi wa kutunga sera ya biashara, ambayo ni kudumisha uwiano kati ya uuzaji na uagizaji bidhaa kutoka nje, kuongeza ushindani na nyongeza ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka nje."

  Kuanzia mwezi wa Januari hadi Novemba mwaka huu, thamani ya mitaji ya nje inayotumia China ilifikia Yuan bilioni 803.62, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 9.8 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na kuvutia makampuni ya nchi za nje kuwekeza nchini China ni mojawapo ya sehemu muhimu za kuhimiza muundo mpya wenye uwazi kamili. Mkutano wa mwaka huu wa kazi za uchumi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umesisitiza tena kupunguza masharti kwa makampuni ya nje kuingia katika soko la China hatua kwa hatua, na kupunguza sekta ambazo haziruhusiwi kuwekezwa na makampuni ya nje. Mfumo wa usimamizi wa orodha ya sekta ambazo haziruhusiwi kuwekezwa na makampuni ya nje unaotekelezwa katika eneo la jaribio la biashara huria la China, ambalo ni eneo la kwanza la majaribio ya biashara huria nchini China umepunguza sekta hizo kutoka 193 hadi 95 kwa sasa, na mfumo huo umefikia kiwango cha uwekezaji wa kimataifa ndani ya miaka minne. Wakati huohuo, Shanghai inafanya jaribio la kujenga bandari ya biashara huria ambayo itapewa mamlaka zaidi ya kujiendesha. Naibu mkurugenzi wa kamati ya kusimamia eneo la biashara huria la Shanghai Lu Fangzhou anaona kujenga bandari ya biashara huria kunalenga kujenga kiwango cha kimataifa cha eneo la biashara huria. Anasema, "Kufanya utafiti wa kujenga bandari ya biashara huria, naona kunalenga kujenga eneo la biashara huria linaloweza kufikia kiwango cha kimataifa, uwazi ambao unahusisha bidhaa, mitaji na wafanyakazi. Hivyo katika mchakato wa utafiti, tumejitahidi sana na tumeacha mamlaka zetu nyingi katika usimamizi."

  Kinachostahili kufuatiliwa ni kuwa mkutano huo umesisitiza kuinua maeneo na ngazi zitakazopewa uwazi, na pia kufungua mawazo, muundo na mfumo wetu. Agizo lililotolewa hivi karibuni na serikali ya China kuhusu kufungua masoko ya benki, dhamana na bima kwa uwekezaji wa nchi za nje pia limeonesha moyo wa mkutano huo. Mtafiti mkuu wa Benki ya China Bw Zong Liang anachambua kuwa kufunguliwa kwa soko la mambo ya fedha sio tu kunaweza kuhimiza sarafu ya RMB kuwa ya kimataifa, bali pia kufanya China iendelee kuwa sehemu inayowekezwa zaidi duniani.Anasema, "Moja ni kulingana na mahitaji ya hali ya nchi, nyingine ni kujenga mazingira mapya ya kibiashara, na kuifanya China kuwa sehemu inayovutia zaidi uwekezaji wa kigeni. Mazingira tunayolenga kujenga ni kuwa, kuja China tu kunaweza kukufanya uchume pesa nyingi zaidi na kuendesha biashara yako nzuri. Tukifanya hivyo tunaweza kupata hali ambapo fedha za nchi za nje zitaendelea kuja China kwa njia sahihi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako