• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kuendelea kutoa mchango katika kuhimiza utatuzi wa suala la Palestina na Israel

    (GMT+08:00) 2017-12-25 19:13:56

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China siku zote inaunga mkono juhudi za wapalestina za kurudisha haki zao halali, na inapenda kuendelea kutoa mchango katika kuhimiza suala la Palestina na Israel lipate utatuzi kamili, wenye haki na wa kudumu, na kutimiza amani katika Mashariki ya Kati.

    Akizungumza kwenye kongamano la tatu la watetezi amani wa Palestina na Israel lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Beijing, Bi Hua Chunying amesema China siku zote inaunga mkono mpango wa kuwepo kwa nchi mbili, na kujenga nchi huru yenye mamlaka kamili ya Palesina katika mipaka ya mwaka 1967, na mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalem Mashariki.

    Ameongeza kuwa China inasisitiza kuwa Palestina ikitimiza kujenga nchi yake, Israel itapata usalama wa kudumu, suala kati ya Palestina na Israel litatatuliwa kwa pande zote, na kuleta utulivu kwenye kanda ya Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako