• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukarabati makazi duni milioni 5.8 mwakani

    (GMT+08:00) 2017-12-25 19:28:35

    China itakarabati makazi duni milioni 5.8 ya aina mbalimbali kwa ajili ya watu maskini nchini humo mwakani.

    Habari hizo zimetolewa kwenye mkutano wa kazi za makazi na ujenzi wa miji na vijiji nchini China uliofanyika jumamosi iliyopita. Waziri wa makazi na ujenzi wa miji na vijiji wa China Wang Menghui amesema kwenye mkutano huo kuwa, mwakani China itasukuma mbele mageuzi, na kuharakisha kujenga sera ya makazi ambayo itazingatia anuwai ya njia za kutoa na kuhakikisha makazi kwa wananchi, na kuwahamasisha kukodisha nyumba mbali na kununua nyumba.

    Wang amesisitiza kuwa, serikali ya China itashikilia msimamo wake kwamba, nyumba ni kwa ajili ya kuishi, si kwa ajili ya kupata faida kwa kupandisha bei, na China itasimamia vizuri soko la nyumba kutokana na aina zake, ili kuhimiza soko hilo kuendelea vizuri na kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako