• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 164 wamefariki baada ya mvua kubwa kunyesha nchini Philippines

  (GMT+08:00) 2017-12-25 20:18:01

  Serikali ya Philippines imesema, watu 164 wamefariki na wengine 171 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha kusini mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

  Mvua kubwa ilianza kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Mindanao ijumaa iliyopita na kusababisha mafuriko ya ghafla na maporomoko ya udongo katika eneo hilo. Watu elfu 98, wengi wakitoka familia za wakulima zenye hali duni ya kiuchumi, walisherehekea sikukuu ya Krismas katika vituo vya uokoaji vilivyowekwa na serikali.

  Tume ya Kudhibiti Majanga nchini humo imesema, baadhi ya wakazi walipuuza wito wa serikali wa kuondoka kwenye maeneo yao kabla ya mvua hiyo kunyesha. Tume hiyo imesema barabara, madaraja, na mashamba yameharibiwa vibaya na mvua hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako