• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia Airlines yataka kuanzisha safari za ndege kwenda Chongqing, China

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:11:50

    Shirika la ndege la Ethiopia linafikiria kuanzisha safari za ndege kwenda Chongqing, mji mkubwa wa kusini magharibi mwa China. Mkurugenzi wa Shirika hilo kanda ya China, Mongolia na Korea Kaskazini Bw. Yared Berta amesema shirika hilo linataka kujiingiza kwenye soko kubwa la usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya China na Afrika. Bw. Berta pia amesema Ethiopia Airlines inataka kuwavutia watalii zaidi wa China kuitembelea Ethiopia ambayo inajitahidi kujijenga kuwa nchi kubwa ya utalii barani Afrika. Hivi sasa Ethiopia Airlines imekuwa na safari za ndege kwenda miji mitano nchini China, yaani Beijing, Hongkong, Shanghai, Chengdu na Guangzhou.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako