Shirika la ndege la Emirates Airline limeamua kusitisha safari za ndege kati ya Tunis na Dubai kuanzia Jumatatu wiki hii, kama ilivyoelekezwa na mamlaka nchini Tunisia. Habari zinasema mgogoro huu ulianza baada ya Emirates kuwazuia wanawake kadhaa wa Tunisia mjini Tunis kupanda ndege yake inayoelekea Dubai wiki iliyopita, kutokana na sababu za kiusalama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |