• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Uganda limesema limewaua wapiganaji 100 wa ADF nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:27:45

    Jeshi la Uganda limesema limewaua wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la ADF kwenye operesheni dhidi ya kundi hilo iliyofanywa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

    Kwenye operesheni iliyotumia ndege na mizinga na kupewa jina la "Tuugo", jeshi hilo lilifanya mashambulizi kwenye kambi kadhaa za kundi hilo, baada ya kupata habari za kijasusi kuwa kundi hilo lilikuwa linajiandaa kufanya mashambulizi. Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limethibitisha kuuawa kwa zaidi ya waasi 100 wa kundi hilo na kambi nane kuharibiwa katika eneo la Eringeti.

    Msemaji wa Operesheni hiyo Meja Ronald Kakurungu amesema kwa sasa wameimarisha usalama mpakani, ili kuhakikisha wapiganaji hao hawavuki mpaka wa Uganda na kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako