• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liberia yaimarisha usalama na ulinzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:44:44

    Polisi ya Liberia wameimarisha usalama na ulinzi nchini kote kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofanyika leo, ili kupunguza hatari ya kutokea kwa vurugu.

    Msemaji wa polisi Bw Sam Collins amewaambia wanahabari mjini Monrovia kuwa uchunguzi umeonyesha kuwa kuna uwezekano mdogo wa kutokea vurugu wakati wa uchaguzi mkuu, na kwamba wana uhakika kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa amani.

    Bw. Collins ameongeza kuwa wamefanya makadirio yote na mipango yote, na wananchi na wageni nchini humo wanaweza kuendelea na kazi zao kama kawaida. Nyota wa Bw Geoge Weah anaonekana kuongoza kwenye kinyang'anyiro hicho, dhidi ya makamu wa rais Bw Joseph Boakai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako