• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan atoa ahadi kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya Sudan na Uturuki

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:51:23

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameahidi kuondoa vikwazo vyote vinavyoathiri uhusiano wa kibiashara kati ya Sudan na Uturuki.

    Rais Al-Bashir alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye jukwaa la kiuchumi la Sudan na Uturuki mbele ya mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

    Rais wa Sudan alitoa mwito wa kuanzishwa kwa benki ya Uturuki nchini Sudan ili kufanikisha biashara kati ya nchi hizo mbili. Pia alitoa wito kuongeza kiasi cha mabadilishano ya kila mwaka kati ya Sudan na Uturuki hadi dola za kimarekani bilioni 10 kutoka milioni 500 za sasa.

    Aidha amesisitiza sekta binafsi za Uturuki ziongeze uwekezaji nchini Sudan na kunufaika na maliasili zilizopo nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako