• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupima na kuchora ramani

    (GMT+08:00) 2017-12-26 10:04:42

    Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupima na kuchora ramani utafanyika mwezi Novemba mwaka kesho mkoani Zhejiang, China.

    Huu utakuwa ni mkutano wa ngazi ya juu zaidi wa kimataifa kuhusu upimaji na uchoraji wa ramani kufanyika nchini China.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Liu Zhenmin, amesema wakati wa mkutano huo washiriki watabadilishana maoni kuhusu maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni katika sekta hiyo, na kutafuta njia za kuunga mkono ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya kuelekea mwaka 2030.

    Kutokana na maendeleo ya teknolojia mpya ikiwa ni pamoja na uongozaji njia wa satelaiti na akili bandia, Umoja wa Mataifa ulianzisha Kamati ya Wataalamu kuhusu uchambuzi wa data za kijiografia kutoka angani mwaka 2011 na kuzindua utaratibu wa uratibu wa kiwango cha juu kati ya serikali za nchi mbalimbali katika sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako