• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa maspika wa nchi sita wafanyika nchini Pakistan

    (GMT+08:00) 2017-12-26 10:05:07

    Mkutano wa maspika wa mabunge ya nchi sita ulifanyika kati ya tarehe 24 hadi 25 Mwezi Desemba mjini Islamabad, Pakistan, kujadili mapambano dhidi ya ugaidi na muunganyiko kati ya nchi hizo, na kupitisha Azimio la Islamabad.

    Naibu spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Ping aliyehudhuria mkutano huo alisema, ugaidi unatishia nchi zote katika kanda hiyo na jumuiya ya kimataifa, na kutokuwa na muunganyiko kati ya nchi kumekuwa ni kikwazo kikubwa kinachozuia maendeleo ya nchi hizo.

    Pia amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali, kuongeza nguvu katika kupambana na ugaidi, kulinda amani na usalama wa kikanda; kuharakisha hatua ya kujenga "Ukanda mmoja, Njia moja", kutimiza mawasiliano kati ya nchi mbalimbali bila matatizo na kupata maendeleo kwa pamoja, ili kuanzisha jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako