• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jambo Jet na Fly 540 zaridhika na hali ya biashara msimu huu wa siku kuu

    (GMT+08:00) 2017-12-26 16:39:57

    Makampuni yanatoa huduma za usafiri wa ndege yanaendelea kuvuna zaidi msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya baada ya kupata pigo kutokana na msukosuko wa kisiasa ulioshuhudiwa hapa nchini Kenya.Kampuni ya ndege ya JamboJet imesema katika kipindi cha uchaguzi iadadi ya abiria ilipungua kwa asilimia 25 huku ile ya Fly540 ikiwa ni asilimia 30.Hata hivyo hivi sasa kampuni hizo mbili za kutoa huduma za usafiri wa angani zimesema idadi ya abiria imeongezeka maradufu na wanatarajia hali itakuwa hivo kipindi chote hiki cha sikukuu.Katibu mtendaji wa kampuni ya Jambo Jet Bwana Willem Hondius amesema hali haikuwa nzuri wakati wa kipindi cha siasa lakini hivi sasa hali ni nzuri. Amesema wateja wengi walikuwa nahofu ya kutokea kwa ghasia katika maeneo mengi kama vile Mombasa, Nairobi na Kisumu.Houndius amesema kutokana na kuongezeka kwa idadi ya abiria, wamelazimika kuongeza safari zao katika miji mingine ya pwani ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako