• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara kati ya China na nchi za nje yaongezeka kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa

  (GMT+08:00) 2017-12-26 17:38:46

  Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, mwaka huu biashara kati ya China na nchi za nje imeongezeka kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa, na kasi ya ongezeko la biashara ya bidhaa ni kubwa zaidi katika miaka 6 iliyopita, huku kasi ya ongezeko la mauzo ya huduma kwa nchi za nje ikiwa kubwa kuliko ile ya yanayoagizwa kutoka nje tangu miaka 7 iliyopita.

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan jana hapa Beijing kwenye mkutano wa kazi za biashara nchini China alidokeza mkakati wa kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu ya kibiashara duniani kabla ya mwaka 2050, na China itachukua hatua mpya katika sekta za matumizi, biashara na uwekezaji kutoka nchi za nje.

  Kwa sasa China inashika nafasi ya mbele duniani katika matumizi ya ndani, biashara na nchi za nje na uwekezaji, na China imekuwa nchi kubwa kiuchumi na biashara. Katika zama mpya, lengo jipya la China ni kuimarisha zaidi hadhi yake ya nchi kubwa kibiashara kabla ya mwaka 2020, kujiendeleza na kuanza kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya kibiashara kabla ya mwaka 2035, na kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya biashara kwa pande zote hadi kufikia mwaka 2050.

  Tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, imepiga hatua kubwa katika biashara kati yake na nchi za nje. Hata hivyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu wa nguvu, uwezo wa uvumbuzi na sifa nzuri ya bidhaa. Mkurugenzi wa idara ya biashara na nchi za nje ya wizara ya biashara ya China Bw. Ren Hongbin amesema, katika siku zijazo China itatimiza mambo ya kisasa katika masoko ya kimataifa na ya ndani, muundo wa bidhaa, mashirika ya uendeshaji, na njia za biashara. Anasema,

  "Tutahimiza mauzo yetu katika nchi za nje kuwa ya mchanganyiko wa bidhaa, huduma, teknolojia na uwekezaji, badala ya bidhaa peke yake; kuhimiza uwezo wetu wa kushindana sokoni kuwa katika teknolojia, vigezo, chapa, sifa na huduma badala ya bei nafuu; kuhimiza injini ya ongezeko la biashara kuwa uvumbuzi badala ya vitu vinavyohitajika katika uzalishaji; kuhimiza mazingira ya biashara kuwa na kiwango cha kimataifa kwa kusanifiwa na mfumo na sheria, badala ya kuelekezwa na sera ya serikali; kuhimiza hadhi ya China kuwa mshiriki wa ubunifu wa utaratibu wa biashara ya kimataifa badala ya mfuasi wa utaratibu huo."

  Takwimu zinaonesha kuwa katika miezi 11 iliyopita ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imezidi dola za kimarekani trilioni 3.8, ambaloni ongezeko la asilimia 15.6 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Wakati huo huo thamani ya biashara ya huduma kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu yuan trilioni 4. Kuhusu hali ya mwakani, Bw. Ren anasema,

  "Hali ya biashara ya kimataifa duniani inakabiliwa na changamoto mbalimbali, kwa vile rais wa Marekani amekanusha hadhi ya soko huria ya China, huku Umoja wa Ulaya ukiendelea kuweka ukaguzi dhidi ya China katika biashara ya kimataifa. Wakati huo huo vitendo vya kujilinda kibiashara na mawazo ya kupinga utandawazi pia vinaleta athari mbaya."

  Hata hivyo Bw. Ren amesisitiza kuwa hali nzuri ya kufufuka kwa uchumi wa dunia, ongezeko la uwezo wa uvumbuzi wa mashirika ya China na sera nzuri za serikali kuu zitahimiza maendeleo ya biashara kati ya China na nchi za nje. Mkurugenzi wa idara ya biashara ya huduma ya wizara ya biashara ya China Bw. Xian Guoyi amesema, katika siku za baadaye China itaharakisha mageuzo ya mfumo na kuboresha mazingira kwenye biashara ya huduma. Anasema,

  "Hatuna uzoefu wengi katika biashara ya huduma. Tunapaswa kukamilisha mfumo wa biashara hiyo katika pande za sheria, sera, takwimu na usimamizi."

  Hivi sasa China inashika nafasi ya tatu duniani katika matumizi ya uwekezaji kutoka nchi za nje. Mwaka kesho, wizara ya biashara ya China itachukua hatua madhubuti ili kuhimiza maendeleo zaidi ya uwekezaji huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako