• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China kwa mwaka huu kuchangia asilimia 57.5 katika ongezeko la uchumi

    (GMT+08:00) 2017-12-26 18:16:18

    Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Wang Zhigang amesema, maendeleo ya teknolojia ya China kwa mwaka 2017 yanaweza kuchangia asilimia 57.5 katika ongezeko la uchumi, na kuifanyia China kuwa karibu na nchi zenye uwezo mkubwa zaidi wa uvumbuzi.

    Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa uchumi wa China, Bw. Wang amesema, kuharakisha kujenga nchi yenye uwezo mkubwa wa uvumbuzi ni hatua muhimu ya kimkakati katika kipindi kipya cha China. Amesema, maendeleo ya teknolojia ni jambo muhimu kwa China kuendelea kuwa nchi yenye nguvu zaidi ya kisasa, bila hivyo itapoteza fursa ya kujiendeleza.

    Bw. Wang pia amesema, katika siku za baadaye, ni muhimu kuendeleza matumizi ya teknolojia mpya na uchumi wa kidijitali, pia ni muhimu kutatua masuala ya upungufu wa wataalam wa juu wa teknolojia na matatizo ya kimuundo ya wavumbzi wa teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako