• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pande tatu wa kuboresha uhusiano kati ya Afghanistan na Pakistan wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-12-26 19:41:21

    Mkutano wa kwanza wa mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za China, Afghanistan na Pakistan umefanyika leo hapa Beijing, na kujadili ajenda tatu za "kuaminiana na kuelewana kisiasa", "maendeleo, ushirikiano na mawasiliano" na "ushirikiano wa usalama dhidi ya ugaidi".

    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema China itatumia utaratibu wa mkutano huo na utaratibu mwingine kutoa mchango wa kiujenzi katika kuboresha uhusiano kati ya Afghanistan na Pakistan. Pia amesema katika mkutano huo, Afghanistan na Pakistan zimekubaliana kuboresha uhusiano wao, kuendeleza ujirani mwema, kutoruhusu mtu yeyote na kundi lolote kutumia ardhi ya nchi moja kupinga na kuharibu nchi nyingine, na kutatua tofauti kupitia mazungumzo.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Afghanitan Khawaja Asif na mwenzake wa Pakistan Salahuddin Rabbani wameshukuru juhudi zinazofanywa na China katika kuchangia maendeleo ya nchi hizo mbili na kuhimiza utulivu wa kikanda, na kusifu pendekezo lililotolewa na China la kuanzisha utaratibu wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako