• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya watu 15 walioshambulia vikosi vya usalama huko Sinai Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-12-26 19:42:11

    Tovuti huru ya habari ya Youm7 nchini Misri imeripoti kuwa magereza nchini humo imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya watu 15 waliothibitishwa kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama katika mkoa wa Sinai Kaskazini.

    Mkoa huo ulioko eneo la jangwa lililo karibu na mpaka wa Misri na Israel na Ukanda wa Gaza wa Palestina umeshuhudia wimbi la mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya polisi na wanajeshi tangu rais wa kiislamu Mohame Morsi kupinduliwa na jeshi mwaka 2013.

    Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri ameapa kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kubwa za kijeshi kutokomeza ugaidi huko Sinai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako