• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, Pakistan na Afghanistan zakubaliana kujadili kurefusha ushoroba wa kiuchumi kati yao

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:21:04

    Mawaziri wa mambo ya nje wa China, Pakistan na Afghanistan jana wamekutana hapa Beijing kujadili mpango wa kurefusha ushoroba wa kiuchumi kati ya China na Pakistani kufika Afghanistan.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema baada ya mkutano kati yake na wenzake wa Pakistani na Afghanistan, kuwa katika siku za baadaye ushoroba wa kiuchumi wa China na Pakistan utaunganishwa na ushoroba wa kiuchumi wa katikati ya China na Asia magharibi.

    Ushoroba wa kiuchumi kati ya China na Pakistan wenye urefu wa kilometa elfu 3, unaanzia mjini Kashgar, magharibi mwa China na kuishia mjini Gwadar, Pakistan, kuiunganisha njia ya hariri ya ardhini na njia ya hariri ya baharini. Miradi yake inayoendelea kujengwa kwa sasa katika upande wa Pakistan ni pamoja na barabara, reli, mabomba ya mafuta na mkonga wa mawasiliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako