• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yatangaza kurejesha mazungumzo na waasi mwezi Januari

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:34:10

    Serikali ya Sudan imetangaza kuwa itarejesha mazungumzo na waasi wa kundi la upinzani SPLM tawi la kaskazini mwezi Januari mwakani mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako pande zote zitajadili mambo kuhusu maeneo ya kusini mwa jimbo la Kordofan na Blue Nile.

    Kiongozi wa ujumbe wa mazungumzo wa serikali ya Sudan Bw Ibrahim Mahmoud Hamid amesema mazungumzo hayo yataanza tena mwezi ujao, na serikali ya Sudan inataka kufikia makubaliano ya amani na waasi hao.

    Ameongeza kuwa serikali ya Sudan inawataka waasi wa kundi la SPLM tawi la kaskazini wabadilishe maoni yao na kutilia maanani mazungumzo hayo, kwa kuwa wananchi wamechoshwa na vita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako