• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika kuzingatia mapambano dhidi ya rushwa

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:46:10

    Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuwa utafanya kikao cha 30 cha kawaida cha wakuu na viongozi wa serikali za nchi wanachama kuanzia tarehe 22 hadi 29 Januari, katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

    Kauli mbiu ya mkutano huo itakuwa "kushinda mapambano dhidi ya rushwa: njia endelevu ya kuelekea mabadiliko ya Afrika". Kutokana na ratiba iliyotangazwa na Umoja wa Afrika, kikao cha 35 cha kawaida cha kamati ya wajumbe wa kudumu (PRC) kitafanyika kuanzia 22 hadi 23 mwezi Januari, na kikao cha 32 cha baraza tendaji kitafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 26 mwezi huo.

    Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika watakutana kutoka tarehe 28 hadi 29 mwezi Januari kwa ajili ya kikao cha 30 cha kawaida cha umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako