• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa Beidou wa China waendelea vizuri katika miaka 5 iliyopita

  (GMT+08:00) 2017-12-27 17:38:51

  Tarehe 27, Desemba mwaka 2012, mfumo wa utambuzi wa maeneo wa satilaiti wa Beidou wa China ulianza kutoa huduma. Katika miaka mitano iliyopita, kutokana na ongezeko mfululizo la uwezo wake, mfumo huo umepanua shughuli zake kwa haraka, na kuiletea China ushirikiano wa kimataifa kwa wingi.

  Mfumo wa utambuzi wa maeneo wa satilaiti wa Beidou wa China unaweza kutoa huduma yenye usahihi wa ngazi ya sentimita, na kuwahudumia wananchi wa China kupitia simu za mkononi na baiskeli za kuchangia matumizi. Mwaka kesho, mfumo huo utatoa huduma kwa kuweka kipaumbele katika nchi zinazojiunga na pendekezo la "ukanda mmoja na njia moja".

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na ofisi ya habari ya baraza la serikali la China, mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa mfumo wa utambuzi wa maeneo wa satilaiti ya China Bw. Ran Chengqi anaona kuwa, mfumo wa Beidou uliendelea vizuri katika miaka mitano iliyopita, huku ukipiga hatua siku hadi siku. Anasema,

  "Katika miaka mitano iliyopita, kikundi cha pili cha satilaiti cha Beidou kimeendelea kufanya kazi vizuri, na usahihi wake umeongezeka na kuwa mita 6 kutoka 10. Kuanzia mwezi Novemba mwaka huu, China itaanza kuunda kikundi cha tatu cha satilaiti, na uwezo wake utakuwa mara mbili ya kikundi cha kwanza."

  Ikilinganishwa na mfumo wa GPS wa Marekani, Glonass wa Russia, na Galileo wa Umoja wa Ulaya, mfumo wa Beidou ni mfumo pekee uliounganisha uwezo wa upashaji wa habari na utambuzi wa maeneo duniani. Bw. Ran amesema mtandao wenye usahihi mkubwa wa utambuzi wa maeneo kutokana na mfumo wa Beidou umekamilika nchini China, na kuwa na uwezo wa kutoa huduma tangu nusu ya kwanza ya mwaka huu. Mtandao huo una usahihi wa ngazi ya sentimita katika baadhi ya maeneo, na utaleta mapinduzi ya huduma za utambuzi wa maeneo duniani. anasema,

  "Watu wengi wanababaishwa na mfumo wa utambuzi wa maeneo kwenye magari yao. Lakini baadaye wakitumia mfumo wenye usahihi mkubwa, makosa hayatatokea tena. Mfumo huo pia utasaidia sana kazi nyingine, kama kukabiliana na ajali za moto. Baadaye huduma ya mfumo huo itapatikana kwa watu nchini China kama huduma za maji na umeme."

  Hivi sasa mfumo wa Beidou unatumiwa katika sekta mbalimbali nchini China zikiwemo usalama wa umma, mawasiliano ya barabarani, uvuvi, umeme, misitu na kupunguza maafa. Mfumo wa Beidou si kama tu ni mfumo wa China, bali pia ni mfumo wa dunia nzima. Bw. Ran anasema,

  "Tumeweka kipaumbele katika nchi zilizojiunga na pendekezo la China la 'ukanda mmoja na njia moja'. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka ujao, China itarusha satilaiti nyingine 18, ili kutoa huduma kwa nchi hizo. Aidha, China itatoa mafunzo na mawasiliano ya teknolojia kwa ajili ya nchi hizo, ili kueneza matumizi ya mfumo wa Beidou."

  Habari zinasema, China itakamilisha mfumo wa Beidou wenye kiwango cha juu zaidi duniani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, na kutoa huduma bora za utambuzi wa maeneo, uongozaji wa safari na kutaja wakati kwa usahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako