• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza Kuu la Umoja wa Matiafa lapitisha bajeti kwa mwaka 2018 na 2019

    (GMT+08:00) 2017-12-27 19:29:37

    Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Matiafa umepitisha azimio la bajeti ya umoja huo kwa mwaka 2018 na 2019 inayofikia dola za Marekani bilioni 5.397, ambayo imepungua kwa dola za Marekani milioni 200 ikilingana na mwaka jana na mwaka huu.

    Bajeti hiyo iliyopendekezwa na kamati ya tano ya umoja huo inayoshughulikia mambo ya mamlaka na bajeti, itatumika katika sekta za kisiasa, utekelezaji wa sheria za kimataifa, ushirikiano wa kikanda, haki za binadamu na habari.

    Habari zinasema, baraza hilo pia limepitisha dola za Marekani milioni 508.49 kwa ajili ya matumizi ya tume 34 za kisiasa zilizotumwa na umoja huo katika nchi mbalimbali, zikiwemo dola za Marekani milioni 82.9 kwa tume nchini Afghanistan na dola za Maerkani milioni 50 kwa tume yake nchini Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako