• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Studio za China zaunda ushirikiano kuboresha usafirishaji wa tamthilia

    (GMT+08:00) 2017-12-27 19:58:02

    Studio kumi za kutengeneza tamthilia nchini China zimeunda ushirikiano ili kwa pamoja kusaidia usafirishaji wa tamthilia za kichina.

    Studio hizo ikiwemo studio inayoongoza kwa burudani Huace Film & TV, H. Brothers na iQIYI, kwa pamoja zimezindua Muungano wa Kusafirisha Tamthilia za Kichina, katika mkutano wa Uvumbuzi wa Sanaa ya Filamu na Televisheni uliofanyika Hangzhou, mkoani Zhejiang mashariki mwa China.

    Mwenyekiti wa Kituo cha Maendeleo cha Utamaduni cha Beijing You Xiaogang amesema, kampuni hizo zimeungana ili kuweza kushirikiana katika jukwaa la kusafirisha tamthilia hizo. Amesema gharama za kusafirisha tamthilia za Kichina ni za chini zaidi kuliko zile zinazotengenezwa nchini Korea Kusini na nchi za Ulaya na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako