• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia 200 zarudi kwenye kambi za wakimbizi kutokana na mashambulizi ya IS huko Kirkuk, Iraq

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:17:39

    Familia 200 zimerudi kwenye kambi za wakimbizi katika mkoa wa Salahudin ulioko katikati ya Iraq, kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Islamic State kuongezeka hivi karibuni kwenye mkoa wa jirani wa Kirkuk. Katika miezi kadhaa iliyopita, mamia ya familia zilirudi makwao kwenye eneo la Hawijah baada ya vikosi vya usalama vya Iraq kuwaondoa wapiganaji wa Islamic State kutoka kwenye vituo vyao kwenye eneo hilo, lakini mashambulizi na mauaji ya hivi karibuni yanayofanywa na waasi wa IS waliobaki, yamezilazimisha familia hizo kukimbia tena nyumba zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako