Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba Bw Antonia Guterres amepongeza duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa Liberia uliofanyika Jumanne kwa amani.
Msemaji wa umoja wa mataifa ameongeza kuwa Bw Guterres amemtuma kiongozi wa zamani wa Nigeria Bw Olusegun Obasanjo kushuhudia makabidhiano ya kwanza ya madaraka ya amani nchini Liberia katika kipindi cha zaidi ya miaka 70. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka maoni ya wapiga kura yaheshimiwe, na makabidhiano hayo ya madaraka yafanyike kama ilivyopangwa.
Duru ya pili ya uchaguzi mkuu ilifanyika Jumanne, na mvutano ulikuwa ni kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na mcheza soka wa zamani wa George Weah.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |