• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Libya mashariki mwa nchi lakaribisha uchaguzi unaokuja

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:45:57

    Msemaji wa jeshi la Libya mashariki mwa nchi Bw. Ahmad Mismari, ametangaza mjini Benghazi kuwa jeshi hilo linakaribisha uchaguzi unaokaribia kufanyika nchini Libya, na kuthibitisha kuwa kazi ya kuandikisha wapiga kura imeanza.

    Amesema uchaguzi huo unatakiwa kuwa na waangalizi wa kimataifa na wa nchi za kiarabu, ili kuhakikisha hakuna upendeleo na uchaguzi uaminike. Amesisitiza kuwa jeshi litalinda vituo vya kupigia kura.

    Uchaguzi huo unafanyika kutokana na mapendekezo yaliyotolewa mwezi septemba na mkuu wa tume ya umoja wa mataifa nchini Libya Bw Ghassan Salame. Mbali na uchaguzi huo, Bw. Salame pia alipendekeza kufanyika kwa mabadiliko ya katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako