• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi 4,500 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakimbilia Uganda

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:46:19

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limesema wakimbizi 4,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamevuka mpaka na kuingia Uganda tangu Desemba 18.

    UNHCR imetoa taarifa ikisema wengi wa waliovuka mpaka na kuingia Uganda walipita ziwa Albert. Habari zinasema wakimbizi walilazimika kutengana na familia zao kutokana na gharama kubwa za kutoka nje ya nchi zinazotozwa na makundi yenye silaha.

    UNHCR pia imesema wakimbizi 3,756 wameelekezwa kwenda Kigoma kwenye makazi ya wakimbizi ya Kyangwali. Asilimia 80 ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto, na mama mmoja mwenye umri wa miaka 70 amefariki baada ya kufika kwenye kituo cha kupokelea wakimbizi kutokana na matatizo ya kiafya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako