• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia amfuta kazi waziri wa mipango ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:55:32

    Rais Edgar Lungu wa Zambia amemfukuza kazi mmoja wa mawaziri wake kwa sababu isiyojulikana.

    Msemaji wa rais Bw. Amos Chanda amesema katika taarifa yake kwamba rais wa Zambia amemfuta kazi waziri wa mipango ya maendeleo Bw. Lucky Mulusa na kumvua ubunge.

    Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja sababu za hatua hiyo.

    Mwezi Oktoba Bw. Mulusa aliwakasirisha wafuasi wa chama tawala kutokana na matumizi ya dola za kimarekani milioni 42 ya zabuni ya vifaa vya zimamoto.

    Hali hii iliwafanya baadhi ya wanachama wa chama tawala kumwandikia ombi na kumshinikiza kiongozi wa Zambia kumfukuza kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako